Pages

Thursday, March 17, 2016

WAZIRI AMPASIKU TATU RC KUUNDA KAMATI YA KUCHUNGUZA VIONGOZI NA WAKUU WA SEKONDARI WANAOLALAMIKIWA KUTUMIA VIBAYA UONGOZI WAO.

 
Na Woinde Shizza, Karatu Vijiji.
WAZIRI waNchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa
Mh,George Simba Chawene amempa siku tatu Mkuuwa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda kuhakikisha anaunda kamati maalumu ambayoitafanya uchunguzi 
kubaini viongozi wa vijiji na wakuu wa sekondari wa wilayaya karatu 
wanaotumia vibaya uongozi wao hali iliyopelekea kuwepo kwamalalamiko.

WaziriSimbachawene aliyasema hayo wakati alipokuwa kwenye uzinduzi wa
majengo ya ofisi na maendelo ya parokia na Karakana ya Chuo cha
Ufundi Audrey Veldamaniliyopo kijiji cha Kitete Wilayani Karatu Mkoani
Arusha ambavyo vinamilikiwa naKanisa katoliki Parokia ya
Kitete.

Alisema kuwakutokana na malalamiko aliyoyapata kutoka kwa
viongozi wa Dini pamoja nawananchi katika Wilaya ya Karatu kuhusiana
na kuwepo kwa baadhi ya viongozi wavijiji na wakuu wa shule za
Sekondari kutumia vibaya uongozi wao ahakikisheanaunda kamati hiyo ili
watakapobaini ukweli waweze kutumbuliwa majipu harakasana.

‘’Mkuu wa Mkoa nakupa siku tatu fatilia jambo hili kuna ubadilifu mwingi upo wizi wafedha wakuu wa shule wamekuwa wakiiba hela za wazazi,ufaulu kwa wanafunziumeshuka sana katika shule zote za Karatu ,viongozi wa
kijiji, kata hawako makini na kazi sasa unda kamati ili tupate
ushahidi wa kudumuili tuwatimue’’alisema Simbachawene.

Pia alimpasiku saba Mkuu huyo wa Mkoa kuhakikisha anashushughulika suala la kuboreshamiundo mbinu hususani barabara ambayo imekuwa kero kubwa kwa 
wakazi wa vijijivi navyozunguka Wilaya ya Karatu akidai kwamba anapaswa 
kukutana na wakurugenziwa monduli na karatu kukutana na kupanga namna 
ya kufungua barabara kuanziaManyara,inayopita sabasaba ,kitete ,Lostete mpaka serera katika kipindi hikicha mwaka huu wa fedha huku akimsihi kuanza kufikiria Barabara ya Namangakupitia Monduli ,ziwa Natron ili iwe ya Mkoa.

Alidai kuwa kuwepo kwa barabara hizo
kutasaidia wananchiwa kufanya biashara zao kwa urahisi huku watalii
wakimiminika kwa wingi jamboambalo litafanya wafanyabiashara kutumia
Raslimali za hapa nchini.

Nae Mkuu waMkoa wa Arusha Felix Ntibenda
alisema kuwa anawasihi viongozi wa Wilaya yaKaratu kuwafanyia kazi
wale watendaji na wenyeviti wanaokwamisha kazi zamaendeleo ya Nchi
kuwafukuza kazi maramoja kabla ya kufika kwake.

‘’Nawambiawakurugenzi na wakuu wa wilaya wafukuzen kazi hao wanaokwenda kinyume na kazitutapata wengine hata kama walichaguliwa na wananchi tambua masuala ya uchaguziyameisha kwisha hakuna chadema wala CCM nisingependa nisikie malumbano bali nikufanya kazi kwa kuheshimu madaraka yaliyoko madarakani’’alisema FelixNtibenda.

Awali akitoahotuba yake mbele ya waziri Paroko waParokia hiyo Padri
Costantine Changwe alisema kuwa katika kijiji cha kitete wananchikwa
ujumla wanakabiliwa na changamoto kubwa ya barabara huku akidai
kwambawakati wamasika huwa wanadondoka makorongoni na wengine kupoteza maisha jamaboambalo limekuwa kero kubwa kwa jamii hiyo.

Alisema kuwakumekuwepo na viongozi wa vijiji na vitongozi wa Mbulumbulu ambao wamekuwa na uongozi mbaya kwa madai kwamba wanalumbana kisiasa hawatakimaendeleo hukuwakipingana na kauli ya hapa kazi .

Alisema kuwawamekuwa wakitanguliza siasa bila uzalendo kwa maslahi yao binafsi huku 
akisemawanapaswa kunyoshewa vidole hata kutumbuliwa majipu jambo 
ambalo litasaidiakuleta maendelea ya wanyonge.

No comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates