Pages

Friday, March 18, 2016

UMOJA WA VYAMA VYA SIASA VISIVYO NA UWAKILISHI BUNGENI VYATOA TAMKO LA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA MAREJEO ZANZIBAR.

 Mwenyekiti wa Makatibu wa  Umoja wa Vyama visivyo na uwakilishi Bungeni, ambae pia ni Katibu wa Chama cha SAU, Ali Kaniki  akizungumza na wandishi wa Habari katika ukumbi wa Studio ya kurikodia Rahaleo kuhusu kushiriki uchaguzi wa marejeo wa Zanzibar tarehe 20 mwezi huu.
Mmoja wa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha TLP Bwana. Hafidh Hassan Suleiman akithibitika wa kugombea na kuwataka wananchi kumpikia kura yeye. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Na waandishi wetu.   Maelezo Zanzibar.
Umoja wa vyama  vya siasa ambavyo havina  uwakilishi Bungeni wametoa tamko rasmi la kushiriki uchaguzi  wa marejeo tarehe 20 mwezi huu na wamewataka wazanzibar kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huo.

Hayo yamezungumzwa na makatibu wakuu wa vyama hivyo wakati walipokuwa wakizungumzwa na waandishi wa habari  katika ukumbi wa studio za Rahaleo  mjini Zanzibar.

Wamesema Chama chochote cha siasa kazi yake ni kushiriki uchaguzi na sio kususia kwani kufanya hivyo kutakoseshawananchi  haki yao ya msingi na  kurudisha nyuma shughuli za maendeleo.

Aidha  wameamua kurejea uchaguzi huo kutokana na kasoro zilizojitokeza uchaguzi wa mwanzo  ambapo  mambo mengi   yalionesha dhahiri  ulikuwa na kasoro za wazi wazi.

 Makatibu hao wamesema kurejewa uchaguzi sio jambo geni duniani  na yapo mataifa mengi yamewahi kurejea uchaguzi kutokana na kasoro mbali mbali zilizojitokeza katika chaguzi zao.

Viongozi wa Umoja huo wamesema  pamoja na kushiriki uchaguzi pia wamesimamisha  wagombea  12 ambao wamo katika ngazi zote ikiwemo rais, wawakilishi na madiwani.

Mwenyekiti wa umoja huo Ali Kaniki amewataka wazanzibari  kujitambua  na kufikra kwani wakiweza kujitambua wataweza kutoa maamuzi yaliyo sahihi.

“Wazanzibar tujitambue kifikra kwani tukiwa tunajitambua tutaweza kutoa maamuzi yalio sahihi, alisema  Kaniki”
Kwa Upande wake  mjumbe wa umoja huo Abdul Mhuya amesema  khatma ya wazanzibar imo mikononi mwa wazanzibar wenyewe  na Tanzania kwa ujumla hivyo wazanzibar wasikubali kuuipoteza thamani yaoya kushiriki kupiga kura kwa kupata viongozi wawatakao.

Vyama vitakavyoshiriki katika marudiao ya uchaguzi huo ni DP,CCK, AFP, DEMOKRASIA MAKINI , SAU, TLP, UPDP, UMD, ADC, NRA, TADEA NA CHAUMMA.

No comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates