Pages

Wednesday, March 16, 2016

SIKU YA UTEPE MWEUPE WA UZAZI SALAMA YAADHIMISHWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akizungumza wakati wa siku ya Utepe Mweupe ambapo na uzinduzi wa kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Pia mama Samia amewasihi wanawake kujiunga na mfuko wa jamii wa bima ya afya ili kusaidia vituo vya afya. Pia amewataka wananchi kuachana na mila potofu hasa za ukeketaji kwani ni kumkosoa mwenyezi Mwenyezi Mungu. 
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Bakari Kambi akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya Upete Mweupo kwa niaba ya Waziri wa Afya maendeleo ya jamii, Jinsia, wazeee na watoto, Ummy Mwalimu leo katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa UNICEF akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya Utepe mweupe  ambapo mama Samia amezindua wa kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto amesema atashirikiana vyema katika kuzuia vifo vya watoto wakati wa kuzaliwa.
 Mwakilishi wa mganga mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Benedict Msiba  akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia vifo vya  mama na mtoto wakati wa kujifungua, ikiwa amesema kuwa katika mkoa wa Rukwa umejitahidi kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
 shuhuda, Efrazia Saidia ambaye amenusurika kifo cha chake na mwanae kutokana na kuumwa uchungu kwa muda mrefu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akionyesha vitabu ambavyo vimezinduliwa leo ambayo ni mpango wa serikali kuendelea  kuchangia  kupunguza vifo vya mama na mtoto.
 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika siku ya Utepe mweupe jijini Dar es Salaam leo na uzinduzi wa mpango mkakati wa kuzuia vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi  wa siku ya Utepe Mweupe leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates