Pages

Wednesday, March 16, 2016

NDEGE MPYA YA MIZIGO YAWASILI ABUDHABI KIJIUNGA NA KITENGO CHA MIZIGO CHA ETIHAD.

KITENGO cha mizigo cha Etihad kimepokea ndege mpya aina ya Boeing 777 ambayo itawezesha kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Etihad kundelea kutanua mipango yake kwa mwaka 2016. Ndege hiyo imekua ya 11 katika kitengo hicho ambapo tayari imeshaanza kazi rasmi Machi 01 mwaka huu.

Kitengo cha mizigo cha Etihad kilitangaza kuwa kingepokea ndege zingine mbili katika maonyesho ya ndege ya Dubai mwaka jana, na kutumia sehemu ya dola bilioni 67 za kimarekani kwa oda iliyotolewa mwaka 2013 kwa ajili ya ndege 199. Ndege hizo mbili zilizoongezwa zina thamani ya dola milioni 637 za kimarekeni na ndege ya pili imewasili Abu Dhabi mwezi huu.

Ndege hizo mpya zitakua na siti tisa ambazo zitaruhusu kitengo hicho cha mizigo cha Etihad kubeba na watu wengine kama sehemu ya mpango wa kubeba farasi wasafirishwao kwa anga, ambayo inasaidia kwa wanyama hao wenye thamani kubwa. Zitakua ndege za kwanza katika kitengo cha mizigo cha Etihad kuwa katika muundo huu. 

Wanyama wasafirishwao kwa anga husimamiwa na mameneja ambao pia husaidiwa na timu ya watunzaji wakiwa angani na pia ardhini, ambapo farasi hao watasafirishwa kwenda sehemu tofauti katika mabara ya Ulaya, Asia, Amerika, Afrika na Australia.

Kevin Knight, Afisa Mkuu wa mipango na mikakati wa shirika la ndge la Etihad alisema, “Ndege iliyoongezwa inatupa fursa ya kutanua kitengo chetu cha mizigo na kukuza soko letu pia. Mwaka uliopita, tuliweza kujitanua katika mabara ya Amerika ya Kusini, Afrika na Asia na ndege hii mpya itaongeza uwezo na kutuwezesha kukua zaidi kwa kupitia mtandao wetu, lakini la muhimu ni pia kuongeza fursa za kukuza mikataba yetu sehemu mbali mbali duniani”.

Mwaka 2015, kitengo cha mizigo cha Etihad kilikuza upatikanaji wake ulimwenguni kwa kutoa huduma katika vituo vipya 6 vya shirika la ndege la Etihad ikiwa ni pamoja na Edinburgh, Madrid na Kolkatta. Etihad sasa inafanya kazi za huduma ya mizigo kwa ratiba maalum katika vituo vya mizigo pekee ambavyo ni; Hahn, San Juan, Bogota, Guangzhou, Dakar, Douala, Eldoret, Hanoi, Houston, Nouakchott, Sharjah na Tbilisi.


Ndege zilizopo kitengo cha mizigo cha Etihad kwa sasa zipo tatu aina ya Boeing 777Fs, Boeing 747s na Airbus A330s. Kitengo hicho cha mizigo cha nchi za umoja wa Kiarabu kwa sasa kinahudumia vituo 14 vya mizigo pekee duniani kote kutoka katika kituo chake kikuu cha Abu Dhabi na ina uwezo wa kubebwa juu ya meli ya shirika la ndege la Etihad yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 100.

“Toka iingie katika huduma miaka 7 iliyopita, ndege ya mizigo 777 imezidi kutambulika kama ndege bora ya mizigo kubwa na bora duniani yenye injini mbili pacha,” alisema Marty Bentrott
Makamu wa Rais wa Mauzo Etihad kwa Mashariki ya Mbali, Urusi, na Asia ya kati. “Tunajivunia kuwa na ndege ya mizigo 777 ikiwa na mchango muhimu katika kitengo cha mizigo cha Etihad wakati ikiendelea kuimarisha na kukuza kitengo hicho sehemu mbali mbali duniani”.

Kitengo hicho cha mizigo cha Etihad huingiza zaidi ya dola bilioni moja kama mapato yake kwa mwaka na kuripotiwa kukua kwa kasi kubwa kwa mwaka 2015 kikiwa na tani 592,090 za mizigo na barua pepe zilizosafirishwa kwa ujumla, ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 4 toka hesabu za mwaka 2014. Kitengo hicho pia ndicho kiini kwa asilimia 88 kwa kuingiza na kusafirisha mizigo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi.

Kikiwa kimeanzishwa mwaka 2004, kitengo cha mizigo cha Eihad ndicho kitengo kikuacho kwa kasi katika kampuni ya ndege ya Etihad. Toka katika kituo chake kikuu kilichopo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi, kitengo cha mizigo cha Etihad kinatoa huduma mbali mbali za mizigo kwa wateja wake kikihusisha na ukuaji wake kimataifa.

No comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates