Pages

Tuesday, March 15, 2016

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA LUPA AKIWA NA DAWA ZA KULEVYA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

· MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA SOME WILAYA YA CHUNYA AUAWA KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIVU WA KIMAPENZI.

· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA LUPA MKOA WA MBEYA AKIWA NA DAWA ZA KULEVYA.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA KITONGOJI CHA KATAVI – B KILICHOPO WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SHIJA PESAMBILI [24] ALIUAWA KWA KUKATWA PANGA MIGUUNI NA MKONO WA KUSHOTO NA MTU AITWAYE MASANJA CHEKA @ DADA.

TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:30 HUKO KITONGOJI CHA MANDA - CHINI, KIJIJI NA KATA YA SOME, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. 

INADAIWA KUWA, MTUHUMIWA ALIMVAMIA SHIJA PESAMBILI WAKATI AKIWA AMELALA PEKE YAKE MAKAMBINI NA KISHA KUANZA KUMKATA PANGA SEHEMU ZA MIGUUNI NA MIKONONI NA KUMJERUHI HALI ILIYOPELEKEA KIFO CHAKE MUDA MFUPI KABLA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI. 

INADAIWA KUWA, CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KIPIGO KILICHOTOKANA NA TUHUMA ZA WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MTUHUMIWA AMBAYE ALITOROKA BAADA YA TUKIO KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA MKE WAKE. UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA MSAKO WA KUMTAFUTA MTUHUMIWA WA TUKIO HILI.

TAARIFA YA MSAKO:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA LUPA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA AITWAYE MAGDALENA ODIRO [21] AKIWA NA DAWA ZA KULEVYA AINA YA BHANGI UZITO WA KILO 01 NA GRAM 700.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.03.2016 MAJIRA YA SAA 17:30 JIONI HUKO KIJIJI NA KATA YA LUPA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO LA MAUAJI AZITOE MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. AIDHA KAMANDA MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates