Pages

Monday, March 21, 2016

WANAFUNZI WASOMEA CHINI KWENYE UDONGO HUKU WAKIFUNDISHWA NA MWALIMU MMOJA.

Na Woinde Shizza,Simanjiro
MPANGO mkakati wa elimu bure kuanzia darasa la Awali mpaka Sekondari umeonekana kutonufaisha baadhi ya walengwa katika maeneo ya pembezeno hususani jamii ya kifugaji  kutoka katika kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambapo wananchi wameamua kumkodisha mwalimu na kumlipa kwaajili ya kufundisha watoto wao.

 Wanafunzi wa shule hii ya msingi Kichagare  wamekuwa wakijisomea huku  wamekaa chini, shule hiyo ikiwa imeezekwa  na vipande vya turubai ili kuweza kupata afueni wakati wakujisomea ambapo lengo la wazazi wao kufanya hivyo ni kuwasaidia watoto wao kupambana na adui ujinga ili kuendana na karne hii ya sasa ya teknolojia.

mwandishi wetu amebahatika kufika eneo la tukio na kuzungumza na mwalimu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la  Lilian Nanyaro ambapo amesema kuwa aliamuakujitolea kufundisha katika shule iliyoko kijiji cha Kichangare kitongoji cha Loongung  hii ikiwa ni kwa ajili ya kuweza kuwapatia wanafunzi na watoto wa kijiji hicho elimu .

Amesema kuwa  mazingira ya shule ya msingi Kichangare ni magumu haswa katika swala zima la ufundishaji kwa hamna vitendea kazi ndani ya shule hiyo ukizingatia  kwamba watoto ambao  ni wanafunzi wana nia ya kutaka kusoma.

‘’ndugu mwandishi kama mnavyoona mazingira ya shule hii yaliyomagumu hamna paa, paa lililopo ndo hivi vipande vya turubai na mengine yametuboka  na pia ukiangalia mazingira ya kijiji chetu mvua zinaponyesha pia inakuwa ni tatizo kubwa sana kwani  inafikia mahali  wanafunzi hushindwa kufika shule kabisa nanapenda kutumia nafasi hii kuomba mbalimbali kuweza kutusaidia tatizo hili kwani iwapo watoto hawa watapata sehemu nzuri ya kusomea itawasadia sana hivo  wadau wajitokeze kutusaidia’’alisema Nanyaro.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo amejitambulisha kwa jina la Seigulu James  amesema kuwa wao kama wanafunzi wanatamani sana kusoma lakini tatizo kubwa walilonalo katika shule hiyo ni madawati hawana, kwani  kwa sasa iviwamekuwa wakikaa chini wakati wakiwa wanasoma.

Ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuwasaidia kuweza kupata angalau madawati pamoja na kuwajengea majengo ya madarasa pamoja na kuwapatia walimu ambao wataweza kuwafundisha ili waweze kupata elimu kama wanafunzi wengine na  watoto wa shule  zingine.

Honie Kimbeye Mkazi wa kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro amesema kuwa wao kama wanakijiji waliamua kukaa na kutafuta mwalimu mmoja ambaye ndio wanae hapo shule ambapo amesema wao kama wanakijiji wanajichangisha ela na kumlipa mwalimu huyo ili aweze kuwafundisha watoto wao.

“sisi tulijikusanya tuka kaa tukaona ni bora tutafute mwalimu ambaye atatusaidia kufundisha watoto wetu hapa kijijini hivyo tunajichanga tunamlipa kila mwisho wa mwezi na kila mzazi amekuwa akichangia shilingi elfu nne kwa ajili ya kumlipa mwalimu huyo”alisema Kimbeye

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Loongung Japhet Losijake amesema kuwa mapaka sasa  tayari  vikao vyao vya bajeti halmashauri wameshaomba kijiji hicho kipewe kipaumbele ili kuweza kuondoa tatizo la ukosefu wa darasa hali inayowafanya watoto kusoma wakiwa chini ya vumbi.

Wahenga wanamsemo usemao usipoziba ufa utajenga ukuta,hivyo ni vyema kama serikali kwa kushirikiana na wizara ya elimu kuangalia eneo hilo kwa ukaribu ili kuweza kuwaondolea changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi n ahata mwalimu kufundisha katika mazingira magumu.

MWANAMKEMMOJA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA MAUAJI YA KIKATILI.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Zubery Muombeja.

MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Frida Kapinga mkazi wa Mkuzo kata ya Msamala mjini Songea  mkoani Ruvuma anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani humo kwa kosa  la kufanya mauaji ya kikatili dhidi ya mtoto wake wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU KUKEMEA MAUAJI YA VIKONGWE NA ALBINO.

MBUNGE wa Viti maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),UPENDO PENEZA amesema kuwa ni uamuzi mzuri uliochukuliwa na kampuni hiyo kwani mkoa huo umekithiri kwa mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu hivyo ni ishara kubwa ya kuelekea kukombolewa.

Peneza alisema kuwa anaamini watu wakimpenda Mungu wataacha kufanya mauaji ya vikongwe na albino na watu wa kawaida, kwani mkoa huo unaongoza kwa mauaji ya aina hii.Alisema Tamasha hilo ni msaada mkubwa kwa mkoa huo kwani litahamasisha na kupinga mauaji huku akisisitiza kuwa kampuni ya Msama ambayo inasifika kusaidia jamii anaiomba pia iwafikie hata watoto wa mitaani wa mkoa wa Geita.

“Tunamshukuru Msama na kamati yake kwani Tamasha linaweza kuwa msaada mkubwa kwa mkoa wetu mauaji yamezidi si kwa walemavu wa ngozi na vikongwe hata watu wa kawaida wanauwawa kwa mapanga na vitu vingine” alisema Peneza.Alitolea mfano wa mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Chadema, Alfonce Mawazo aliyeuwawa kwa kukatwakatwa mapanga hivyo kupitia tamasha la pasaka litawaasa waache mauaji.

“Kupitia hili Tamasha naamini wataacha vitendo hivyo kwa sababu Mungu anasema tusiue, mpende mwenzio, kwa hiyo mimi nadhani tamasha hili liwe la kihistoria kwa ajili ya kuwataka na kumrudia mungu,” anasema. Peneza alisema asiwe Msama tu hata asasi, kampuni na wadau mbalimbali wajitokeze kupinga mauaji kwani hilo ni janga la kitaifa.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEKELEZA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA LA KUHAKIKI SILAHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwa makini zoezi la uhakiki wa silaha zake lililokuwa likifanywa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Rais amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi Silaha aina ya Bastola Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi silaha aina ya shortgun Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiiweka silaha yake vizuri mara baada ya kuhakikiwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

KUMBUKUMBU YA MIAKA 5 YA MZEE JOHN LUWANDA

Baba wa Mzee BEDA

TRL YASITISHA SAFARI ZA KUANZIA DAR ES SALAAM, WASAFIRI WA MWANZA NA KIGOMA SASA KUANZIA SAFARI ZAO MKOANI DODOMA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Reli Nchini (TRL) imesitisha safari zake kutoka Dar es salaam kwenda Mikoani na kuhamishia huduma hiyo mkoani Dodoma kutokana miundombinu ya reli kuharibiwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini. 

Mvua hizo zimeharibu miundombinu ya reli ya kati wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Kaimu Mkurugenzi TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa kutokana na kusitishwa kwa huduma hiyo ratiba ya huduma mpya inatarajiwa kuanza kesho Machi 22 kwa wasafiri wanaotarajia kusafiri kutoka Dodoma kwenda Mwanza na Kigoma kuanzia majira ya  saa 11 jioni.

Amesema gari moshi jipya ya Delux kwa wasafiri wa Kigoma wanatakiwa kukata stakabadhi ya malipo ya safari siku ya Jumanne saa 2:00.

Kadogosa amesema kuwa jitihada mbalimbali zinaendelea kufuatia mashirikiano kati ya kampuni hodhi ya Rahco pamoja na Shirika la reli nchini ili kuweza kurejesha huduma hiyo kama ilivyokuwa awali.

Amesema kuwa wasafiri wanaotumia usafiri huo waondowe wasiwasi kutokana na jitihada zinazofanywa za urejeshaji wa huduma ya reli.

Saturday, March 19, 2016

BREAKING NEWSSSS.. RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI TATU ZA SERIKALI.

 
 Dkt. Ayoub Rioba ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Prof. Godius Kahyarara ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Friday, March 18, 2016

WACHINA WA KAGASHEKI WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA.

 Raia wa Kichina kutoka kulia ni na Xu Fujie na  Huang Jing  ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela au kulipa faini ya shilingi bilioni 54 leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Raia wa kichina wakisindikizwa na Askari Magereza mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Raia wa China wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 au kulipa zaidi ya sh.bilioni 54 kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya makosa mawili.

Washitakiwa hao katika kosa la kwanza ni kukutwa ni kuwa na nyara ya serikali ya vipande vya meno ya tembo 706 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni tano na kosa la pili kushawishi kutoa rushwa kwa askari sh.milioni 30.

Washitakiwa hao ni Huang Jing pamoja na Xu Fujie wameanza kutumikia kifungo hicho leo baada ya kushindwa kutoa faini hiyo.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu         Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Sprian Mkeya amesema kuwa kutokana na kupata maelezo katika pande zote mbili pamoja na kuisababishia hasara serikali washitakiwa adhabu yao ni miaka 30 au kulipa  ya zaidi ya bilioni tano (5).

Hakimu Mkeya amesema washitakiwa hao wanaweza kukata rufaa makahakama kuu kutokana na hukumu iliyotoka.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba mahakama iwape adhabu kali kutokana na kosa waliolifanya na kudai kuwa kutokana na kukamatwa kwao vitendo vya uhalifu kwa wanyamapori vimepungua
Kwa upande wa Wakili upande wa washitakiwa Nehemia Mkoko aliomba mahakama kuwaonea huruma kwa adhabu wataoipata ili waweze kutoka na kuweza kujumuika na familia zao. Washitakiwa hao walikamatwa 2010 katika eneo la mikocheni mwaka huu.

UAMUZI WA RAIS MAGUFULI KUTOA ELIMU BURE UTACHOCHEA USAWA WA KIJINSIA NCHINI – UMMY MWALIMU

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.)wakati akitoa taarifa ya nchi katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake Duniani (CSW).

Mhe Ummy alieleza kuwa Adhma ya Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutoa Elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari itakuwa na matokeo makubwa ya kuongeza udahili wa wanafunzi katika Elimu ya msingi, Sekondari na Elimu ya juu.

Akaongeza kwamba uimarishwaji wa upatikananaji wa elimu kwa wanawake ni msingi mkubwa wa kuwezesha wanawake kiuchumi, kwakuwa elimu hutoa ujuzi, maarifa na hali ya kujiamini kwa wanawake kuendea fursa za kiuchumi.Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ( Mb) akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu dhima ya uwezeshwaji wa wanawake na uhusiano wake na utekelezaji wa Agenda 2030. katika mchango wake Waziri anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake amesema Serikali inatambua umuhimu wa mwanamke katika utekelezaji wa ajenda mpya ya maendeleo endelevu ( Agenda 2030) na kwamba itaendelea kumwezesha.

Katika Taarifa hiyo, Mheshimiwa Waziri, alieleza kuwa Serikali ya Tanzania inatambua kuwa uwezeshaji wa wanawake na Usawa wa jinsia unachangia kwa kiasi kikubwa kufikiwa kwa wepesi kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu ( Sustainable Development Goals). Kwa kutambua hilo Tanzania imejipanga kuhuisha Ajenda 2030 katika Sera, Sheria na Mipango ya nchi kwa kuhakikisha kunakuwa wa sheria zinazolenga kuleta Usawa wa Jinsia na uwezeshaji wa wanawake, ambapo pamoja na mambo mengine utekelezaji wa Mikakati, Sera na Sheria utaendelea kuzingatia haki ya kielimu kwa Wanawake na Wasichana.

Mheshimiwa Ummy, aliongelea pia umuhimu wa Afya kwa wanawake na Wasichana (ikiwa ni pamoja kupunguza vifo vya wajawazito na watoto) kama njia ya kumuwezesha mwanamke kushiriki kikamilifu katika uzalishaji mali.

Mkutano huo wa wiki mbili unafanyika NewYork, Marekani kuanzia tarehe 14-24 Machi 2016, ukihusisha wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubadilishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo Serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.


Mheshimiwa Ummy Mwalimu akiwa pamoja na Mhe. Balozi Tuvako Manongi na Mhe Peter Serukamba (Mb.), mara baada ya kuwasilisha taarifa ya Tanzania kuhusu Masuala ya Maendeleo ya Wanawake.

UMOJA WA VYAMA VYA SIASA VISIVYO NA UWAKILISHI BUNGENI VYATOA TAMKO LA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA MAREJEO ZANZIBAR.

 Mwenyekiti wa Makatibu wa  Umoja wa Vyama visivyo na uwakilishi Bungeni, ambae pia ni Katibu wa Chama cha SAU, Ali Kaniki  akizungumza na wandishi wa Habari katika ukumbi wa Studio ya kurikodia Rahaleo kuhusu kushiriki uchaguzi wa marejeo wa Zanzibar tarehe 20 mwezi huu.
Mmoja wa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha TLP Bwana. Hafidh Hassan Suleiman akithibitika wa kugombea na kuwataka wananchi kumpikia kura yeye. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Na waandishi wetu.   Maelezo Zanzibar.
Umoja wa vyama  vya siasa ambavyo havina  uwakilishi Bungeni wametoa tamko rasmi la kushiriki uchaguzi  wa marejeo tarehe 20 mwezi huu na wamewataka wazanzibar kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huo.

Hayo yamezungumzwa na makatibu wakuu wa vyama hivyo wakati walipokuwa wakizungumzwa na waandishi wa habari  katika ukumbi wa studio za Rahaleo  mjini Zanzibar.

Wamesema Chama chochote cha siasa kazi yake ni kushiriki uchaguzi na sio kususia kwani kufanya hivyo kutakoseshawananchi  haki yao ya msingi na  kurudisha nyuma shughuli za maendeleo.

Aidha  wameamua kurejea uchaguzi huo kutokana na kasoro zilizojitokeza uchaguzi wa mwanzo  ambapo  mambo mengi   yalionesha dhahiri  ulikuwa na kasoro za wazi wazi.

 Makatibu hao wamesema kurejewa uchaguzi sio jambo geni duniani  na yapo mataifa mengi yamewahi kurejea uchaguzi kutokana na kasoro mbali mbali zilizojitokeza katika chaguzi zao.

Viongozi wa Umoja huo wamesema  pamoja na kushiriki uchaguzi pia wamesimamisha  wagombea  12 ambao wamo katika ngazi zote ikiwemo rais, wawakilishi na madiwani.

Mwenyekiti wa umoja huo Ali Kaniki amewataka wazanzibari  kujitambua  na kufikra kwani wakiweza kujitambua wataweza kutoa maamuzi yaliyo sahihi.

“Wazanzibar tujitambue kifikra kwani tukiwa tunajitambua tutaweza kutoa maamuzi yalio sahihi, alisema  Kaniki”
Kwa Upande wake  mjumbe wa umoja huo Abdul Mhuya amesema  khatma ya wazanzibar imo mikononi mwa wazanzibar wenyewe  na Tanzania kwa ujumla hivyo wazanzibar wasikubali kuuipoteza thamani yaoya kushiriki kupiga kura kwa kupata viongozi wawatakao.

Vyama vitakavyoshiriki katika marudiao ya uchaguzi huo ni DP,CCK, AFP, DEMOKRASIA MAKINI , SAU, TLP, UPDP, UMD, ADC, NRA, TADEA NA CHAUMMA.

WAANDISHI WA HABARI KUTOKA NCHINI FINLAND WATEMBELEA TAASISI YA UONGOZI.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja (wapili kutoka kushoto) akizungumza na kundi la waandishi wa habari kutoka nchini Finland (hawapo pichani) mapema leo walipotembelea taasisi hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen, Mshauri wa masuala ya Ushirikiano kutoka Taasisi ya UONGOZI Bi. Liisa Tervo na Mkuu wa Utafiti na Sera kutoka Taasisi ya UONGOZI Bw. Dennis Rweyemamu. 
 Kundi la waandishi wa habari 15 kutoka nchini Finland waliotembelea Taasisi ya UONGOZI mapema leo ikiwa ni moja kati ya mafunzo yao katika programu maalum ya maendeleo na sera inayoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland. Waandishi hao ambao wapo nchini kwa muda wa siku tano pia walisindikizwa na watumishi wawili kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland.
 Mratibu wa programu ya Maliasili Bi. Namwaka Omari (kulia) akitoa mada kwa waandishi hao wa habari kuhusu namna Taasisi ya UONGOZI inachangia katika kuimarisha usimamizi wa maliasili zetu nchini hususan katika sekta ya mafuta na gesi.
 Mmoja kati ya waandishi hao akiuliza swali. Baadhi ya mada zilizogusiwa katika mazungumzo ni pamoja na jinsi gani Tanzania inatekeleza dhana ya maendeleo endelevu, uimarishaji wa uwezo kwa viongozi barani Afrika, uchumi wa sekta ya gesi nchini na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi ya UONGOZI katika mazingira ya Serikali Mpya.
Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen (kushoto) akitoa neno lake la shukrani kwa niaba ya waandishi wa habari na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, walipotembelea Taasisi ya UONGOZI kufahamu shughuli zake mapema leo. 

KAMPUNI YA HUSEA YASHEREKEA KUTIMIZA MWAKA MMOJA NA AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA LEO KATIKA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya Husea imeadhimisha mwaka mmoja tangu kuazishwa kwake Machi mwaka huu kwa kutoa msaada wa vifaa vya hospitali na kuwapa zawadi akinamama waliojifungua leo katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wandishi wetu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Husea, Pamela Maro amesema kuwa Kampuni hiyo inajishughulisha na Mipango miji, utoaji ushauri bure kuhusiana na Ardhi, Upimaji wa Ardhi pamoja na uchoraji ramani za nyumba, pia amesema kuwa ofisi za Kampuni ya kampuni ya Husea zipo Sinza Palestina kwa yeyote anayetaka ushauri kuhusiana na ardhi anaweza kufika maeneo hayo kujipatia ushauri bila malipo.

Pia Pamera amewaasa wanawake waliotoka kujifungua leo na wanawake wote wanaopenda kumiliki ardhi kisheria waende katika ofisi zao ili waweze kupata ushauri wa bure kuhusiana na maswala ya ardhi.

Kwa upande wa Daktari Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza, Wandi Kariame amewapongeza wafanyakazi wa  kampuni ya Husea kwa kuadhimisha mwaka mmoja leo .

Pia amewashukuru kwa  kuona mahitaji ya Hospitali hiyo na kuwapongeza wanawake waliojifungua leo kwa kuwapa zawadi ikiwa ni kuadhimisha siku iliyofunguliwa ofisi hiyo kwa kufikisha mwaka mmoja wa kampuni hiyo kwani wangeweza kwenda  katika hospitali nyingine au kwenda kilabu cha  pombe (Bar) kwenda kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni yao kwa kunjwa na kula vitu wanavyovitaka tuu lakini wamewaona wao.
Mratibu Huduma Tiba katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Palestina Sinza, Faith Mdee akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Husea inayojishughulisha na utoaji ushauri, upimaji wa viwanja, uchoraji ramani za nyumba pamoja na mipango miji.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Husea, Pamela Maro akimkabidhi Daktari Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza, Dkt. Wandi Kariame  aadhi ya vifaa vinavyotumika katika uzalishaji katika wodi la wazazi katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Muuguzi katika wodi ya wazazi katika hospitali Palestina Sinza.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hosea, Pamela Maro  pamoja na madaktari wa hospitali ya Palestina Sinza wakimkabidhi baadhi ya zawadi zilizotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Husea, mama aliyotoka kujifungua katika hospitali hiyo, Bahati Ramadhani.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Husea akimwangalia mtoto aliyetoka kuzaliwa masaa machache yaliyopita. 
 Baadhi ya wazazi wakiwa wamewapakata watoto waliojifungua leo mara baada ya kupata zawadi na kampuni ya Husea jijini Dar es Salaam leo.


Mfanyakazi wa Kampuni ya Husea akimkabidhi mama aliyetoka kujifungua mda mfupi kabla ya kupewa zawadi hiyo katika hospitali ya Palestina Sinza leo jijini Dar es Salaa.
 Mfanyakazi wa kampuni ya Husea akimkabidhi mama aliyejifungua kwa njia ya Operesheni katika hosipitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam.
 Mama na mwana wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Husea, Pamela Maro(Kushoto) akiwa na baaadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Husea katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa zawadi kwa watoto walipozaliwa leo katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni hiyo tangu kuanzishwa.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
 
 
Blogger Templates