Social Icons

Pages

Featured Posts

Monday, March 21, 2016

WANAFUNZI WASOMEA CHINI KWENYE UDONGO HUKU WAKIFUNDISHWA NA MWALIMU MMOJA.

Na Woinde Shizza,Simanjiro
MPANGO mkakati wa elimu bure kuanzia darasa la Awali mpaka Sekondari umeonekana kutonufaisha baadhi ya walengwa katika maeneo ya pembezeno hususani jamii ya kifugaji  kutoka katika kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambapo wananchi wameamua kumkodisha mwalimu na kumlipa kwaajili ya kufundisha watoto wao.

 Wanafunzi wa shule hii ya msingi Kichagare  wamekuwa wakijisomea huku  wamekaa chini, shule hiyo ikiwa imeezekwa  na vipande vya turubai ili kuweza kupata afueni wakati wakujisomea ambapo lengo la wazazi wao kufanya hivyo ni kuwasaidia watoto wao kupambana na adui ujinga ili kuendana na karne hii ya sasa ya teknolojia.

mwandishi wetu amebahatika kufika eneo la tukio na kuzungumza na mwalimu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la  Lilian Nanyaro ambapo amesema kuwa aliamuakujitolea kufundisha katika shule iliyoko kijiji cha Kichangare kitongoji cha Loongung  hii ikiwa ni kwa ajili ya kuweza kuwapatia wanafunzi na watoto wa kijiji hicho elimu .

Amesema kuwa  mazingira ya shule ya msingi Kichangare ni magumu haswa katika swala zima la ufundishaji kwa hamna vitendea kazi ndani ya shule hiyo ukizingatia  kwamba watoto ambao  ni wanafunzi wana nia ya kutaka kusoma.

‘’ndugu mwandishi kama mnavyoona mazingira ya shule hii yaliyomagumu hamna paa, paa lililopo ndo hivi vipande vya turubai na mengine yametuboka  na pia ukiangalia mazingira ya kijiji chetu mvua zinaponyesha pia inakuwa ni tatizo kubwa sana kwani  inafikia mahali  wanafunzi hushindwa kufika shule kabisa nanapenda kutumia nafasi hii kuomba mbalimbali kuweza kutusaidia tatizo hili kwani iwapo watoto hawa watapata sehemu nzuri ya kusomea itawasadia sana hivo  wadau wajitokeze kutusaidia’’alisema Nanyaro.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo amejitambulisha kwa jina la Seigulu James  amesema kuwa wao kama wanafunzi wanatamani sana kusoma lakini tatizo kubwa walilonalo katika shule hiyo ni madawati hawana, kwani  kwa sasa iviwamekuwa wakikaa chini wakati wakiwa wanasoma.

Ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuwasaidia kuweza kupata angalau madawati pamoja na kuwajengea majengo ya madarasa pamoja na kuwapatia walimu ambao wataweza kuwafundisha ili waweze kupata elimu kama wanafunzi wengine na  watoto wa shule  zingine.

Honie Kimbeye Mkazi wa kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro amesema kuwa wao kama wanakijiji waliamua kukaa na kutafuta mwalimu mmoja ambaye ndio wanae hapo shule ambapo amesema wao kama wanakijiji wanajichangisha ela na kumlipa mwalimu huyo ili aweze kuwafundisha watoto wao.

“sisi tulijikusanya tuka kaa tukaona ni bora tutafute mwalimu ambaye atatusaidia kufundisha watoto wetu hapa kijijini hivyo tunajichanga tunamlipa kila mwisho wa mwezi na kila mzazi amekuwa akichangia shilingi elfu nne kwa ajili ya kumlipa mwalimu huyo”alisema Kimbeye

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Loongung Japhet Losijake amesema kuwa mapaka sasa  tayari  vikao vyao vya bajeti halmashauri wameshaomba kijiji hicho kipewe kipaumbele ili kuweza kuondoa tatizo la ukosefu wa darasa hali inayowafanya watoto kusoma wakiwa chini ya vumbi.

Wahenga wanamsemo usemao usipoziba ufa utajenga ukuta,hivyo ni vyema kama serikali kwa kushirikiana na wizara ya elimu kuangalia eneo hilo kwa ukaribu ili kuweza kuwaondolea changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi n ahata mwalimu kufundisha katika mazingira magumu.

MWANAMKEMMOJA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA MAUAJI YA KIKATILI.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Zubery Muombeja.

MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Frida Kapinga mkazi wa Mkuzo kata ya Msamala mjini Songea  mkoani Ruvuma anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani humo kwa kosa  la kufanya mauaji ya kikatili dhidi ya mtoto wake wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU KUKEMEA MAUAJI YA VIKONGWE NA ALBINO.

MBUNGE wa Viti maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),UPENDO PENEZA amesema kuwa ni uamuzi mzuri uliochukuliwa na kampuni hiyo kwani mkoa huo umekithiri kwa mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu hivyo ni ishara kubwa ya kuelekea kukombolewa.

Peneza alisema kuwa anaamini watu wakimpenda Mungu wataacha kufanya mauaji ya vikongwe na albino na watu wa kawaida, kwani mkoa huo unaongoza kwa mauaji ya aina hii.Alisema Tamasha hilo ni msaada mkubwa kwa mkoa huo kwani litahamasisha na kupinga mauaji huku akisisitiza kuwa kampuni ya Msama ambayo inasifika kusaidia jamii anaiomba pia iwafikie hata watoto wa mitaani wa mkoa wa Geita.

“Tunamshukuru Msama na kamati yake kwani Tamasha linaweza kuwa msaada mkubwa kwa mkoa wetu mauaji yamezidi si kwa walemavu wa ngozi na vikongwe hata watu wa kawaida wanauwawa kwa mapanga na vitu vingine” alisema Peneza.Alitolea mfano wa mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Chadema, Alfonce Mawazo aliyeuwawa kwa kukatwakatwa mapanga hivyo kupitia tamasha la pasaka litawaasa waache mauaji.

“Kupitia hili Tamasha naamini wataacha vitendo hivyo kwa sababu Mungu anasema tusiue, mpende mwenzio, kwa hiyo mimi nadhani tamasha hili liwe la kihistoria kwa ajili ya kuwataka na kumrudia mungu,” anasema. Peneza alisema asiwe Msama tu hata asasi, kampuni na wadau mbalimbali wajitokeze kupinga mauaji kwani hilo ni janga la kitaifa.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEKELEZA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA LA KUHAKIKI SILAHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwa makini zoezi la uhakiki wa silaha zake lililokuwa likifanywa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Rais amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi Silaha aina ya Bastola Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi silaha aina ya shortgun Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiiweka silaha yake vizuri mara baada ya kuhakikiwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

KUMBUKUMBU YA MIAKA 5 YA MZEE JOHN LUWANDA

Baba wa Mzee BEDA

TRL YASITISHA SAFARI ZA KUANZIA DAR ES SALAAM, WASAFIRI WA MWANZA NA KIGOMA SASA KUANZIA SAFARI ZAO MKOANI DODOMA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Reli Nchini (TRL) imesitisha safari zake kutoka Dar es salaam kwenda Mikoani na kuhamishia huduma hiyo mkoani Dodoma kutokana miundombinu ya reli kuharibiwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini. 

Mvua hizo zimeharibu miundombinu ya reli ya kati wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Kaimu Mkurugenzi TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa kutokana na kusitishwa kwa huduma hiyo ratiba ya huduma mpya inatarajiwa kuanza kesho Machi 22 kwa wasafiri wanaotarajia kusafiri kutoka Dodoma kwenda Mwanza na Kigoma kuanzia majira ya  saa 11 jioni.

Amesema gari moshi jipya ya Delux kwa wasafiri wa Kigoma wanatakiwa kukata stakabadhi ya malipo ya safari siku ya Jumanne saa 2:00.

Kadogosa amesema kuwa jitihada mbalimbali zinaendelea kufuatia mashirikiano kati ya kampuni hodhi ya Rahco pamoja na Shirika la reli nchini ili kuweza kurejesha huduma hiyo kama ilivyokuwa awali.

Amesema kuwa wasafiri wanaotumia usafiri huo waondowe wasiwasi kutokana na jitihada zinazofanywa za urejeshaji wa huduma ya reli.

Saturday, March 19, 2016

BREAKING NEWSSSS.. RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI TATU ZA SERIKALI.

 
 Dkt. Ayoub Rioba ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Prof. Godius Kahyarara ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
 
 
Blogger Templates